Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation

Web Name: Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation

WebSite: http://foreigntanzania.blogspot.com

ID:209671

Keywords:

Foreign,Affairs,Ministry,of,African,Cooperation,and,East,

Description:

keywords:
description:
Wednesday, October 20, 2021 SERIKALI YAZIHAKIKISHIA KAMPUNI ZA UFARANSA MAZINGIRA SALAMA UWEKEZAJI

Na Mwandishi Wetu, Dar

Tanzaniaimezihakikishia Kampuni za Kifaransa kuwa mazingira ya biashara na uwekezaji nisalama na kuwasihi kuwekeza kwa wingi hapa nchini.

Akiongeana Waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika kwa kongamano lililowakutanishaMawaziri wa Kisekta, wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ufaransa Jijini Dares Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, BaloziLiberata Mulamula (Mb) amesema Serikali imewahakikishia wafanyabishara nawawekezaji wa kampuni za Kifaransa kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inajenga nainaendelea kuboresha mazingira rafiki ya uwekezaji kwa kuondoa kero mbalimbalizilizokuwa zinawakabili wawekezaji hapa nchini.

Serikaliya Awamu ya Sita iko serious.. na tuna azma kubwa ya kuhakikisha kwambatunajenga mazingira rafiki ya kuweza kuwekeza na kuondoa kero zote ambazozimekuwa zinajitokeza.na makampuni mengine yameeleza hizo kero lakinitunafurahi kuona kero hizo tayari zimeanza kuondolewa, amesema Balozi Mulamula

BaloziMulamula ameongeza kuwa Wafaransa wamekuwa na uhusiano mzuri na Tanzania kwamuda mrefu na hivi sasa wamekuwa na shauku ya kufanya biashara na kuwekeza kwawingi hapa nchini..ambapo takwimu zinaonesha watalii kutoka Ufaransa kujaTanzania kila mwezi ni zaidi ya watalii 7000 wanaokuja kutembelea vivutiombalimbali hapa nchini, hivyo ni changamoto kwetu kuchangamkia fursa hiiadhimu.

Kwaupande wake, Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe.Franck Riester amesema Ufaransa inatambua jitihada zinazofanywa na Serikali yaTanzania ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji mamboambayo pia yanatiliwa mkazo na serikali ya Ufaransa.

Ufaransaimedhamiria kuongeza ushirikiano na Tanzania na kama mlivyoshuhudia leotumeanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka Paris hadi Zanzibar ambaoulisimama tangu mwaka 1974, huu ni mwanzo mzuri amesema Mhe. Riester

Mhe.Riester ameongeza kuwa wataendelea kuwaeleza na kuwahamasisha wafanyabiasharana wawekezaji wa Ufaransa juu ya fursa mbalimbali zinazopatika Tanzania ikiwemokatika sekta ya Nishati, Utalii, Viwanda, Usafirishaji pamoja na Uwekezaji ilikuja kuwekeza na kukuza ucbumi wa pande zote mbili.

Mawaziriwa Kisekta waliohudhuria kongamano hilo ni Waziri wa mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb), Waziri wa Maliasilina Utalii Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), Waziri wa Nishati, Mhe. JanuaryMakamba (Mb) Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb)Waziri wa Uwekezaji Zanzibar Mhe. Mudrick Soraga, Waziri wa Viwanda naBiashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) na Waziri wa Ofisi ya Rais UwekezajiMhe. Geoffrey Mwambe (Mb).

Kampunizilizoshiriki katika kongamano hilo ni pamoja na; CMA-CGM, Bolloré, Airbus, Thales,Lagardére, Total, Chama cha Wafanyabiashara wa Ufaransa-Tanzania, Engie pamojana Maurel Prom.

Waziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula(Mb) akiongea na washiriki wa Kongamano lililowakutanisha Mawaziri wa Kisekta, wafanyabiasharana wawekezaji kutoka Ufaransa Jijini Dar es Salaam


Waziriwa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester akiongeana washiriki wa Kongamano lililowakutanisha Mawaziri wa Kisekta, wafanyabiasharana wawekezaji kutoka Ufaransa Jijini Dar es Salaam


Mawaziriwa Kisekta pamoja na Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ufaransa wakiendeleana Kongamano Jijini Dar es Salaam


Mawaziriwa Kisekta pamoja na Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ufaransa wakiendeleana Kongamano Jijini Dar es Salaam


Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ufaransa wakiendeleana Kongamano Jijini Dar es Salaam


Waziriwa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester akiongeana waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumalizika kwa Kongamanolililowakutanisha Mawaziri wa Kisekta, wafanyabiashara na wawekezaji kutokaUfaransa Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianowa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb)


Waziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula(Mb) akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa Kongamanolililowakutanisha Mawaziri wa Kisekta, wafanyabiashara na wawekezaji kutokaUfaransa Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Biashara za Kimataifa naUwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester



No comments: RAIS NDAYISHIMIYE WA BURUNDI KUZURU TANZANIA

Raiswa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye, anatarajiwa kuwasili nchini kwa ziara ya Kitaifa ya siku tatu kuanzia tarehe 22 hadi 24 Oktoba, 2021.

Akiongeana Waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. BaloziLiberata Mulamula amesema Mhe. Rais Ndayishimiye atawasili katika uwanja wandege wa Dodoma tarehe 22 Oktoba na kuelekea Ikulu ya Chamwino ambako atapokelewarasmi na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Waziri Mulamula amesema baada ya kuwasili Ikulu ya Chamwino,Rais Ndayishimiye atakagua gwaride la heshima na kupigiwa mizinga 21 kwaheshima yake na baadae viongozi hao watakuwa na mazungumzo ya faragha nakufuatiwa na mazungumzo rasmi.

Balozi Mulamula amesema akiwa jijini Dodoma tarehe 22 Oktobamchana, Mhe.Rais Ndayishimiye atatembelea na kuweka jiwe la msingi katikakiwanda cha kuzalisha mbolea ya asili yenye mchanganyiko wa madini ya phosphatena samadi kinachojengwa katikaeneo la viwanda la Nala, kiwanda ambacho kinajengwa na Wawekezajiwa kampuni ya Itracom Fertilizers Limited(ITRACOM) kutoka nchini Burundi na baadaye jioniatahudhuria dhifa ya kitaifa itakayofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

BaloziMulamula ameongeza kuwa tarehe 23 Oktoba 2021 Mhe. Rais Ndayishimiye ataelekeaZanzibar ambako atapokelewa na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi nakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake huyo na baadaye ataelelekea Mkoani Dar esSalaam ambapo ataungana na mwenyeji wake Mhe. Rais Samia .

Amesemaakiwa jijini Dar es Salaam Rais Ndayishimiye anatarajiwa kutembelea Bandari yaDar es Salaam na kukagua ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) unaoendelea nchinikutokea stesheni ya Dar es salaam hadi stesheni ya Kwala - Ruvu pamoja na kutembelea bandari kavu ya Kwalainayojengwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania katika eneo hilo la Kwala mkoaniPwani ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa bandari kavu hiyo.

Akizungumziaziara hiyo ya Rais Ndayishimiye nchini, Balozi Mulamula amesema ni mwendelezo wa hatuazinazochukuliwa na Serikali za Tanzania na Burundi za kuimarisha uhusiano naushirikiano kwa maslahi ya pande zote na itaendeleza na kukuza ushirikianouliopo na kufungua fursa ya kuanzisha maeneo mingine ya ushirikiano ikiwa nipamoja na kuwawezesha Waheshimiwa Marais hao (wa Tanzania na Burundi) kufahamuhatua zilizofikiwa katika kutekeleza maagizo yao waliyoyatoa wakati wa ziara yaMhe. Rais Samia Suluhu Hassan aliyoifanya nchini Burundi tarehe 16 na 17Julai, 2021.

Balozi Mulamula amesemaMhe. Rais Ndayishimiye na ujumbe wake wanatarajiwa kuondoka nchini kurejeaBurundi tarehe 24 Oktoba 2021 baada ya kumaliza ziara yake.


No comments: Tuesday, October 19, 2021 UFARANSA KUKARABATI UWANJA WA NDEGE TERMINAL TWO

Na Mwandishi Wetu, Dar

Tanzaniana Ufaransa zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika maeneo ya kimkakatiikiwemo Nishati, Elimu, Kilimo na Miundombinu ambapo Ufaransa imekubalikukarabati Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal Two JijiniDar es Salaam

Waziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula(Mb) ameyasema hayo wakati akizungumza na Waziri wa Biashara za Kimataifa naUwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester leo alipowasili Jijini Dar es Salaamkwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Kumekuwana Miradi ambayo Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lao la Maendeleo wamekuwawakifadhili Miradi mbalimbali katika Sekta mbalimbali hapa nchini zikiwemosekta za Nishati, Elimu, Kilimo na Miundombinu.

Mtakumbukakuwa Ufaransa ndiyo waliojenga Uwanja wa Ndege wa Termirnal Two wa Julius KambarageNyerere sasa wanakuja na mradi wa kukarabati uwanja huo na kuufanya kuwa wakisasa zaidi. Sasa hivi tu terminal three lakini terminal two imekuwa ikitumikana ndege zinazofanya safari zake za ndani hapa nchini..mradi huu ni moja katiya mradi mkubwa na utakamilika hivi karibuni.

Waziriwa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester yuponchini Tanzania kuzindua safari za Shirika la ndege la Ufaransa Fance Airlinekutoka Parishadi Zanzibar ambapo mara ya mwisho kwa shirika hilo kufanya safari zake hapanchini ilikuwa mwaka 1974.

Septemba15, 2021 Balozi wa Ufaransa hapa nchini Mhe. Nabil Hajlaouvi alisema Serikaliya Ufaransa kupitia Shirika lake la ndege Fance Airline inategemea kuanzishasafari mpya ya ndege kutoka Ufaransa moja kwa moja hadi Zanzibar kuanzia 19Oktoba 2021.

Katikatukio jingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Liberata Mulamula (Mb) ametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyewahikuwa waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Colin Powell.

Kwakweli Serikali ya Tanzania tumeshtushwa sana na kifo chakekatika kipindichake aliendeleza uhusiano wa Marekani na Mataifa mbalimbali, kwa kweli nimasikitiko makubwa tutamkumbuka daima, Amesema Balozi Mulamula

Waziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi LiberataMulamula (Mb) akisalimiana na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji waUfaransa, Mhe. Franck Riester leo alipowasili katika Uwanja wa Ndege waKimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi ya sikumoja


Waziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi LiberataMulamula (Mb) (wa saba kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri waBiashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester (kushotokwa Balozi Mulamula) na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (watano kutoka kulia) pamoja na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali katikaUwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ziaraya kikazi ya siku moja


Waziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi LiberataMulamula (Mb) akiongea na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji waUfaransa, Mhe. Franck Riester katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JuliusNyerere Jijini Dar es Salaam


Waziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi LiberataMulamula (Mb) akiongea na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji waUfaransa, Mhe. Franck Riester katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JuliusNyerere Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Prof. Makame Mbarawa (Mb).


Maongezabaina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. BaloziLiberata Mulamula (Mb) na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji waUfaransa, Mhe. Franck Riester yakiendelea. Maongezi hayo pia yamehudhuriwa naWaziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikianowa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine, Balozi wa Tanzania Nchini Ufaransa Mhe.Samwel Shelukindo, Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe. Nabil Hajlaouvi pamojana viongozi mbalimbali.


KatibuMkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi JosephSokoine, (kulia) akiwa na Balozi wa Tanzania Nchini Ufaransa Mhe. Samwel Shelukindo,pamoja na Mkurugezi wa Idara ya Amerika na Ulaya Balozi Swahiba Mndeme wakifuatilia kikao cha Waziri Mulamula na Waziriwa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester (hawapopichani) leo Jijini Dar es Salaam


Waziriwa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester akielezajambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. BaloziLiberata Mulamula (Mb) pamoja na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. MakameMbarawa leo Jijini Dar es Salaam


Waziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi LiberataMulamula (Mb) akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro Waziri waBiashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester leo JijiniDar es Salaam


Mawaziriwakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi leo Jijini Dar es Salaam



No comments: TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUIMARISHA MISINGI YA DIPLOMASIA

Na Mwandishi wetu, Dar

Tanzania na Chinazimeahidi kuendelea kuimarisha misingi ya uhusiano wa diplomasia baina yamataifa hayo iliyodumu kwa zaidi ya miaka 50 kwa lengo la kukuza na kuendelezamaendeleo endelevu kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Ahadi hiyo imetolewa na Baloziwa China hapa nchini, Mhe. Chen Mingjian, wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula(Mb) leo jijini Dar es Salaam.

Balozi Mulamula amesemakuwa pamoja na mambo mengine, wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo suala la kukuzana kuendeleza misingi ya uhusiano wa kidiplomasia iliyowekwa wakati wakuanzisha mahusiano ya kidiplomasia baina ya mataifa haya 1964.

Uhusiano wa Tanzania naChina ni wa muda mrefu na umekuwa imara katika nyakati zote hii ni kutokana nakila taifa kuheshimu misingi ya taifa jingine na kutokuingilia masuala ya ndaniya taifa jingine, naamini kwa kuzingatia misingi hii uhusiano huu utaendeleakukua na kuimarika zaidi, Amesema Balozi Mulamula

Balozi Mulamula ameongezakuwa wakati wote Tanzania na China zimekuwa na maelewano mazuri ambayoyamechangia kuimarisha diplomasia kwa mataifa hayo.

Balozi wa China hapa nchini,Mhe. Chen Mingjian, ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano ambao imekuwaikimpatia tangu aliwasili na kuongeza kuwa China itaendelea kushirikiana naTanzania katika kukuza na kuendeleza ushirikiano wa kufanya kazi kwa pamoja kwamanufaa ya mataifa mawili.

Naamini kuwa mimi nikiungo cha kuimarisha na kuendeleza uhusiano baina ya China naTanzania..tumekuwa tukishirikiana katia sekta mbalimbali ikiwemo afya, kilimo,biashara na uwekezaji, miradi ya mikopo nafuu na misaada, Teknolojia ya Habarina Mawasiliano (TEHAMA), Uchukuzi, Utalii na utamaduni naahidi kuwa Chinaitaendelea kushirikiana na Tanzania kwa maslahi mapana ya pande zote mbili,Amesema Balozi Mingjian

Waziri wa Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiongea naBalozi wa China hapa nchini Mhe. Chen Mingjian wakati walipokutana kwamazungumzo leo katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam


Balozi wa China hapa nchini Mhe.Chen Mingjian akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa AfrikaMashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati walipokutana kwa mazungumzo leokatika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Mazungumzo baina ya Waziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb)na Balozi wa China hapa nchini Mhe. Chen Mingjian yakiendelea katika OfisiNdogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Mazungumzo baina ya Waziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb)na Balozi wa China hapa nchini Mhe. Chen Mingjian yakiendelea katika OfisiNdogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Balozi wa China hapa nchini Mhe.Chen Mingjian akimkabidhi zawadi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano waAfrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara jijiniDar es Salaam

No comments: Monday, October 18, 2021 TANZANIA, KENYA KUMALIZA VIKWAZO VYA KIUTAWALA DISEMBA

Na Mwandishi Wetu, Dar

Tanzaniana Kenya zimedhamiria kumalizia kuondoa vikwazo vya kiutawala vilivyosaliaifikapo Disemba 2021 baada ya kuondoa vikwazo 46 visivyokuwa vya kikodi.

Hayoyamesemwa wakati wa mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianowa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) na Balozi wa Kenya NchiniTanzania Mhe. Dany Kazungu jijini Dar es Salaam ambapo takwimu zinaonesha urariwa biashara kati ya Nchi hizo umeongezeka mara sita zaidi baada ya kuondolewakwa vikwazo hivyo.

Kutokanana hatua hiyo, Tanzania imeonekana kunufaika zaidi kwa kuondolewa kwa vikwazohivyo kwa kuuza zaidi bidhaa zake nchini Kenya.

Hiini ishara nzuri kwa Tanzania lakini pia ni fursa kwa Tanzania na Kenya kuondoaumaskini kwa watoto wetu na ndugu zetu kupata ajira kwa wingi katika sekta yabiashara, Amesema Mhe. Kazungu

PiaBalozi Kazungu amemueleza Waziri Mulamula kuhusu azma ya Rais wa Kenya Mhe.Uhuru Kenyatta kufanya ziara rasmi hapa nchini na kisha kuhudhuria sherehe zaUhuru tarehe 9 Disemba 2021 ambapo alialikwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipotembelea Kenya mapema mwaka huu.

Waziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamulaamesema Tanzania inaheshimu makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa awali wakuondo vikwazo hivyo na dhamira ni kuwa ifikapo Disemba 2021 vikwazo vyakiutawala navyo viwe vimeondolewa ili kukuza zaidi mahusiano ya Kidiplomasia naBiashara baina ya Tanzania na Kenya.

Tumekubalianakuhakikisha ifikapo mwezi Disemba 2021 vikwazo vyote vya kitawala viwe vimetatuliwa.azmayetu ni kuhakikisha kuwa kila kitu kinakuwa sawa kwa Ustawi wa Diplomasia nabiashara baina ya Tanzania na Kenya, amesema Balozi Mulamula.

Katikatukio jingine, Balozi Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Mwakilishi waTaasisi ya Sister Cities ya Marekani Bi. Ronda Pierce katika Ofisi Ndogo zaWizara Jijini Dar es Salaam

Baloziwa Kenya Nchini Tanzania Mhe. Dany Kazungu akiongea na Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) walipokutanakwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara leo Jijini Dar es Salaam


Waziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi LiberataMulamula (Mb) akimuleleza jambo Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mhe. DanyKazungu walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara leo Jijini Dares Salaam


Mazungumzobaina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. BaloziLiberata Mulamula (Mb) na Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mhe. Dany Kazungu yakiendeleakatika Ofisi ndogo za Wizara leo Jijini Dar es Salaam


Mwakilishiwa Taasisi ya Sister Cities ya Marekani Bi. Ronda Pierce akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianowa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) walipokutana kwamazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara leo Jijini Dar es Salaam


Mazungumzobaina ya wakilishi wa Taasisi ya Sister Cities ya Marekani Bi. Ronda Pierce na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianowa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) yakiendelea katikaOfisi ndogo za Wizara leo Jijini Dar es Salaam



No comments: Friday, October 15, 2021 NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI ATETA NA BALOZI WA CHINA HAPA NCHINI

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) aakiwa katika mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa Nchini Balozi Chen Mingjian.
Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amekumbushia utekelezwaji wa ahadi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang Yi ya kuipa Tanzania masoko ya bidhaa za asali na mabondo, ahadi aliyoitoa Chato Mkoani Geita mwezi Januari,2021 wakati wa ziara yake hapa nchini


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa Nchini Balozi Chen Mingjian mara baada ya kumaliza mazungumzo.

No comments: VACANCY ANNOUNCEMENT AT THE CONSULATE OF THE REPUBLIC OF KENYA IN ARUSHA, TANZANIA.


CLICK HERE TO OPEN THE LINK

No comments: Thursday, October 14, 2021 BALOZI MBAROUK ATETA NA DKT. MATHUKI

NaibuWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi MbaroukNassoro Mbarouk (Mb) amekutana kwa mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya yaAfrika Mashariki, Dkt. Peter Mathuki leo katika Ofisi za Jumuiya hiyo leo JijiniArusha.

NaibuWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi MbaroukNassoro Mbarouk (Mb) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya AfrikaMashariki, Dkt. Peter Mathuki leo katika Ofisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, JijiniArusha


Naibu Waziri wa Mambo yaNje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk (Mb) akisainikitabu cha wageni katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,Dkt. Peter Mathuki leo katika Ofisi za Jumuiya hiyo Jijini Arusha
Naibu Waziri wa Mambo yaNje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk (Mb) akisainikitabu cha wageni katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,Dkt. Peter Mathuki leo katika Ofisi za Jumuiya hiyo Jijini Arusha
Katibu Mkuu wa Jumuiya yaAfrika Mashariki, Dkt. Peter Mathuki akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mambo yaNje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk (Mb) leokatika Ofisi za Jumuiya hiyo Jijini Arusha

No comments: Afrika yajiandaa kuzalisha chakula cha kutosha

Afrikayajiandaa kuzalisha chakula cha kutosha

Na. Mwandishi Maalum, Addis Ababa

Mkutano wa 39 waKawaida wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Umoja wa Afrika umefunguliwa leojijini Addis Ababa, Ethiopia ambapo pamoja na mambo mengine, Mawaziri watapitiaAndiko na mikakati ya utekelezaji wa kaulimbiu ya Mwaka 2022 ya Lishe naUsalama wa Chakula barani Afrika. Kaulimbiu hiyo inalenga kusisitiza umuhimuwa lishe bora kwa ajili ya ukuaji na ustawi wa watoto barani Afrika, baraambalo kwa miaka mingi limekuwa linakabiliwa na uzalishaji mdogo wa chakula. Hivyo, nchi za Afrika zinashauriwa kutekelezamapendekezo ya Progarmu ya Afrika ya Maendeleo ya Kilimo na Azimio la Malabokuhusu kilimo ili kuondokana na changamoto ya lishe duni.

Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula anaongoza ujumbewa Tanzania katika mkutano huo na katika mijadala yake, pamoja na mambo mengine,anatarajiwa kusisitiza umuhimu wa kukifanya Kiswahili kuwa moja ya lugha yakazi katika Umoja wa Afrika.

Mhe. Mulamula atakumbushana kulisisitiza suala hilo kwa sababu limeainishwa katika kaulimbiu ya mwaka2021 ambayo pamoja na mambo mengine, imehimiza matumizi ya lugha za kiafrika naKiswahili ni moja ya lugha hizo ambayo inakuwa kwa kasi na kuzungumzwa na watuwengi barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Aidha, WaheshimiwaMawaziri watapokea taarifa kuhusu ugonjwa wa UVIKO-19 ambapo katika hotuba yaufunguzi ya Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri ambaye ni Waziri wa Mambo ya Njewa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo alisistiza umuhimu wa nchi wanachamakuzingatia tahadhari za maambukizi ya UVIKO-19 ikiwa ni pamoja na kuhamasishawatu wao kupata chanjo ya ugonjwa huo, huku jitihada zikiendelea kuhakikishakuwa nchi za Afrika zinapata idadi ya kutosha ya chanjo kwa ajili ya watu wake.

Katika Mkutano huo pia,Mawaziri wa Mambo ya Nje watapitia na kupitisha bajeti ya Mwaka 2022 yaKamisheni ya Umoja wa Afrika na kufanya uchaguzi wa nafasi mbalimbali zauongozi, zikiwemo za makamishna wawili wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Rais naMakamu wa Rais wa Chuo Kikuu cha Pan Africa, wajumbe wanne wa Kamisheni yaUmoja wa Afrika ya Haki za Binadamu na Watu na wajumbe wanne wa Bodi ya Ushauriya Afrika ya Kupambana na Rushwa.

Vile vile, Mkutano wa39 wa Mawaziri utapitia na kupitisha miundo ya taasisi saba za Umoja wa Afrika,ukiwemo muundo wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara barani Afrika ambaloTanzania imeridhia Mkataba wake hivi karibuni. Kupitishwa kwa miundo hiyoitakuwa ni fursa zikiwemo za ajira kwa nchi wanachama, hivyo, Balozi Mulamulaamewataka Watanzania kuzichangamkia, pindi zitakapotangazwa.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (kushoto) na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Bi. Eliza Rwitunga wakiwa katika kikao cha kujiandaa na ujumbe wa Tanzania kabla ya kuingia kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Umoja wa Afrika.


Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akisoma hotuba ya ufunguzi katika Mkutano wa 39 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Afrika unaofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 14 na 15 Oktoba 2021
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz (kulia) na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Caroline Chipeta wakisikiliza hotuba ya ufunguzi yaMkutano wa 39 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Afrika unaofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 14 na 15 Oktoba 2021

Ujumbe wa Tanzania katika kikao cha maandalizi naWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
ujumbe wa Tanzania ukijumuisha maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia wakiwa katika kikao cha maandalizi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula.

Picha ya pmoja ya Mawaziri wa nchi za Umoja wa Afrika wanaoshiriki Mkutano wa 39 wa Kawaida wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za AU jijini Addis Ababa, Ethiopia.


No comments: Older PostsHomeSubscribe to:Posts (Atom)ForeignTZ Blog App
Lets connect
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mhe. Balozi Liberata MulamulaSubscribe To Foreign Tanzania NewsPosts Atom PostsAll Comments Atom All CommentsMy Blog ListMICHUZIDIT YASHUKULIWA KWA KUHAMASISHA WASICHANA KUSOMA SAYANSI NJOMBE2 hours agoIKULU BLOGWherever To Market Your Movies On-line2 years agoJUMUIYA IMARAVacancy Announcemnt5 years ago
About MeForeignTanzaniaView my complete profileFollowersAwesome Inc. theme. Powered by Blogger.Blog Archive 2021(257) October(22)SERIKALI YAZIHAKIKISHIA KAMPUNI ZA UFARANSA MAZING...RAIS NDAYISHIMIYE WA BURUNDI KUZURU TANZANIAUFARANSA KUKARABATI UWANJA WA NDEGE TERMINAL TWOTANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUIMARISHA MISINGI YA DIP...TANZANIA, KENYA KUMALIZA VIKWAZO VYA KIUTAWALA DIS...NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFR...VACANCY ANNOUNCEMENT AT THE CONSULATE OF THE REPUB...BALOZI MBAROUK ATETA NA DKT. MATHUKIAfrika yajiandaa kuzalisha chakula cha kutoshaBalozi Bana awapokea Wanajeshi watakao shiriki Mic...EALA WAKUTANA MKUTANO WA KWANZA JIJINI ARUSHATANZANIA YAPONGEZWA KUFANIKISHA MAONESHO YA UTALII...Sekta zaidi nchini kunufaika na mikopo nafuu ya Be...WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MA...TANZANIA, CZECH ZAAHIDI KUIMARISHA BIASHARA NA UWE...JAMHURI YA CZECH YAKABIDHI VITANDA VIWILI VYA KISA...WAFANYABIASHARA, WAWEKEZAJI KUTOKA CZECH WAONYESHA...BALOZI MULAMULA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MKURUGEN...UBALOZI WA TANZANIA NCHINI NAMIBIA WAANDAA MAONYES...Mwenyekiti Mtendaji wa Shell ateta na Balozi wa Ta...WAZIRI MULAMULA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 61 Y...WAZIRI MULAMULA AWAAGA MABALOZI WALIOMALIZA MUDA W... September(26) August(23) July(30) June(37) May(37) April(20) March(28) February(20) January(14) 2020(247) December(27) November(22) October(15) September(21) August(15) July(18) June(25) May(20) April(7) March(27) February(32) January(18) 2019(378) December(22) November(31) October(33) September(33) August(34) July(24) June(27) May(44) April(29) March(47) February(22) January(32) 2018(354) December(12) November(38) October(33) September(24) August(35) July(19) June(29) May(42) April(48) March(19) February(31) January(24) 2017(276) December(19) November(25) October(20) September(11) August(15) July(26) June(22) May(29) April(20) March(25) February(42) January(22) 2016(410) December(21) November(38) October(34) September(28) August(42) July(34) June(46) May(35) April(23) March(44) February(30) January(35) 2015(420) December(34) November(30) October(44) September(44) August(29) July(27) June(38) May(28) April(44) March(37) February(36) January(29) 2014(350) December(28) November(16) October(35) September(31) August(32) July(47) June(33) May(31) April(26) March(21) February(17) January(33) 2013(493) December(27) November(53) October(45) September(50) August(47) July(47) June(33) May(47) April(32) March(47) February(31) January(34) 2012(342) December(21) November(28) October(44) September(70) August(34) July(64) June(21) May(4) April(16) March(17) February(13) January(10) 2011(61) December(16) November(31) October(7) September(5) August(1) July(1)

TAGS:Foreign Affairs Ministry of African Cooperation and East 

<<< Thank you for your visit >>>

Websites to related :
Tienda online de muebles de dise

  keywords:tiendas on,diseño tiendas on,tiendas on diseño y tendencias,muebles de diseño tiendas on,mueble comedor,tiendas decoración,muebles coloni

pjsr.org

  keywords:
description:

Modern Essentials | Modern Furni

  keywords:modern furniture, modern rugs, modern bedroom furniture, modern dining furniture, modern lighting
description:Shop Modern Essentials for mode

KESTA & SOMOMAR

  keywords:
description:
EspañolEnglishFrançais

Kaleem Salahuddin - GTA HOMES FO

  keywords:Home ,VAUGHAN real estate, VAUGHAN Ontario real estate, VAUGHAN mls listings, VAUGHAN homes, VAUGHAN homes for sale, VAUGHAN mls listings, VA

Leon Levy Native Plant Preserve

  keywords:
description:

ArchWare - Download Free Softwar

  keywords:
description:
About Sitemap Contact Form Request SoftwareMENU Menu Home Games Android Games PPSSPP Games PS3 PS4 PC GamesActionAdventureFigh

Google 翻译

  keywords:翻译, 译文, 翻译器, 翻译助手, 译者, 机器翻译, 在线翻译
description:Google 的免费翻译服务可提供简体中文和另外 100 多种语言之间的互译功能,可让您

hitchhikingteens.net

  keywords:
description:

RapeFactor.net

  keywords:
description:RapeFactor - download rape porn, forced sex, necro xxx, japanese girl raped and much more for free. The RapeFactor is the world

ads

Hot Websites