BONGO CELEBRITY | All You Wanted To Know But Didnt Know How and Where

Web Name: BONGO CELEBRITY | All You Wanted To Know But Didnt Know How and Where

WebSite: http://bongocelebrity.wordpress.com

ID:182489

Keywords:

You,Wanted,To,

Description:

Zimetanda habari za kushtua kidogo.Habari zinapasha kwamba mtuhumiwa Amatus Liyumba(pichani) ametoweka,hajulikani aliko na heka heka za kumsaka kwa udi na uvumba ndio zimeshaanza? Waliomdhamini wameshaanza kukiona cha moto.Ilikuwaje?Kaenda wapi?Ni kweli?Bonyeza hapa kujua zaidi.Comments (1)Majuzi wakati ulimwengu unasheherekea sikukuu ya wapendanao,mtangazaji maarufu nchini Tanzania,Michael Maluwe alihitimisha siku hiyo kwa kufunga ndoa na kipenzi chake Diana katika Kanisa Katoliki Parokia ya Msimbazi jijini Dar-es-salaam.Pichani ni Michael na Diana wakati wa tafrija iliyofanyika katika ukumbi wa Sunset uliopo Mbezi jijini Dar-es-salaam.BC inawatakia ndoa bora yenye Baraka na maelewano tele.Picha hii ni kwa hisani ya Father Kidevu ambaye kama unamuhitaji kwa shughuli yako unaweza kumpata kupitia simu yake namba +255 755 373999.Hakuna ubishi kwamba kijana Hamis Mwinjuma au maarufu kama MwanaFalsafa(MwanaFA) ni miongoni mwa wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya ambao wamefanikiwa.MwanaFA amefanikiwa sio tu kufikisha ujumbe alioukusudia kwa jamii bali pia kuwa na uwezo wa kuendesha maisha yake kupitia muziki.Miziki yake imekuwa ikiimbwa na watu wa rika mbalimbali.Hayo nayo ni mafanikio.Pamoja na mafanikio ya kimuziki au kisanii aliyonayo MwanaFA,anabakia kuwa mfano wa kuigwa linapokuja suala zima la elimu,muziki na maisha.Hivi karibuni alithibitisha hilo pale alipoamua kurejea tena shule.Safari hii ameelekea nchini Uingereza.Nini kinamsukuma kijana huyu katika nyanja ya elimu? Na je hivi karibuni alipoachia wimbo unaokwenda kwa jina Msiache Kuongea alikuwa anamjibu Inspekta Haruni?Anazungumziaje maisha ya nchini Uingereza?Fuatana nasi katika mahojiano haya mafupi na MwanaFABC: Pamoja na mafanikio mazuri katika muziki kule Bongo bado umeamua kurudi tena shule.Nini kinakusukuma?Hapo UK umeenda kusomea nini na katika chuo gani?FA: Kuna mengi yanafanya nifanye nnachofanya.Lakini kubwa na la msingi zaidi ni kuwa na nguzo nyingine kwa ajili ya maisha ninayoishi(Plan B).Kama unavyojua muziki pamoja na kuwa unakwenda vizuri lakini hautabiriki sana.Ni ngumu kujihakikishia nafasi ya moja kwa moja kwa angalau miaka 10 ijayo.Na zaidi ni kuwa naona kama kuna muda mwingi kama msanii wa kibongo nakuwa naupoteza kwa kutofanya chochote baada ya kurekodi(ambayo sio kila siku),kufanya shows(mara nyingi huwa weekends),matangazo(mara chache kama una bahati) na interviews ambazo nazo sio kila siku.Kwa hiyo kwenye wiki kunakuwa na muda mwingi unaenda bure ambao nimeona ni vyema nikautumia kufanya kitu kitakachozalisha.Hapa UK nasoma Msc Finance na nipo Coventry University.BC: Una mpango gani na muziki kwa hivi sasa?Kama utaendeleza muziki na shule vilevile,lini labda wapenzi watarajie albamu yako mpya? (more )Comments (30)Leo ni siku ya wapendanao duniani au maarufu kama Valentine s Day.Ni sikukuu ambayo zamani ilikuwa ya kimagharibi zaidi kabla ya kuenea ulimwenguni kote.Sina mengi sana zaidi ya kuwaambieni wasomaji na watembeleaji wote wa BC kwamba tunawapenda na tunawatakia sikukuu njema.Enjoy!Comments (4)Katika medani ya soka nchini Tanzania,inaaminika kwamba kama wewe sio mshabiki wa Yanga(Watoto wa Jangwani) basi ni mshabiki wa Simba(Wekundu wa Msimbazi).Hivyo ndivyo ambavyo imekuwa tangu enzi na enzi.Kwa upande wa muziki wa dansi,inaaminika kabisa kwamba kama wewe sio mnazi wa Sikinde basi ni wa Msondo.Utashi na ushindani uliopo katika muziki wa dansi ni sawa kabisa na ule uliokuwepo katika soka la bongo.Haishangazi basi kusikia kwamba uvumi ulipoenea jijini Dar-es-salaam mapema wiki hii kwamba DDC Mlimani Park Orchestra imesambaratika,habari hiyo haikuwa nzuri hata kidogo kwa mashabiki wa muziki nchini Tanzania achilia mbali wanazi wa Sikinde.Hakuna ambaye alitaka kuamini kwamba inawezekana ikawepo Msondo bila Sikinde.Lakini sio kweli kwamba Sikinde ndio imefikia tamati.Kilichotokea ni kwamba kumekuwepo hali ya kutoelewana katika mambo fulani fulani baina ya uongozi wa DDC(Shirika la Maendeleo la Dar-es-salaam) ambao ndio walikuwa wamiliki wa bendi hiyo na hivyo kuitwa DDC Mlimani Park Orchestra).Matokeo yake ni kwamba bendi hiyo,kuanzia tarehe 1 Machi mwaka huu itaanza kujiendesha yenyewe bila usimamizi wala udhamini wa DDC.Na kuanzia hapo watajulikana kama Mlimani Park Orchestra. Kwa hiyo mashabiki wa muziki wa dansi,Sikinde bado ipo!Naam baada ya ufafanuzi huo,leo ni mwanzo wa weekend.Hapa kwetu BC ni kama jadi.Ni wakati wa zilipendwa.Wiki hii kwa upande wangu binafsi imekuwa ngumu kidogo.Imekuwa na maudhi ya haja.Si unajua inavyokuwa pale unapomthamini mtu na kujaribu kumtendea kila aina ya wema unaoweza lakini yeye akakuona kama kinyesi tu?Inaudhi eenh?Basi hali hiyo ndiyo iliyonikumba.Ni vurumai za maisha ambazo kwa kweli huwa natamani zingekuwa na suluhisho la kudumu!Bahati nzuri ni kwamba zipo nyimbo kama hii ya leo ya Maneno Maneno kutoka kwao wana Sikinde,ambayo inaweza kusaidia pindi joto la nyikani linapojiri.Hakuna haja ya maneno.Inafikia mahala lazima utulie na kumuachia Mola.Usikilize wimbo huu kwa makini lakini wakati huo huo usisahau kujirusha .Kibao hiki kitabakia kuwa mojawapo ya kumbukumbu nzuri za Sikinde wakiwa kama DDC Mlimani Park Orchestra.Tunawatakia kila la kheri katika safari yao mpya kama Mlimani Park Orchestra.Tunaamini kwamba Sikinde will always be Sikinde.Ciaohttps://bongocelebrity.files.wordpress.com/2009/02/ddc-mlimani-park-maneno-maneno-mp31.mp3Picha ni kundi zima la wanamuziki wa Mlimani Park Orchestra kabla ya kuanza kwa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar mapema wiki hii.Picha na John Bukuku.Comments (7)Tunapenda kuwajulisha ya kuwa Mzee Leonard NJ Merere ambaye pia ni baba mzazi wa ndugu zetu Naomi na Jacob[JJ] Merere wa Boston-Masachusetts amefariki dunia siku ya Jumanne [Feb 10th 2009] asubuhi hapa Boston,USA.Marehemu alikuwa  na umri wa miaka 73, ameacha mjane,watoto watatu na wajukuu wanne.Taratibu na mipango ya  kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Dar es salaam kwa mazishi zinafanyika nyumbani kwa watoto wake huko Boston-Masachusetts.Kila mmoja wetu anaombwa kuchangia fedha kwa ajili ya kuwezesha kusafirisha mwili wa marehemu kurudi nyumbani kwa mazishi.Gharama za kuhifadhi mwili,kusafirisha mwili,Jeneza pamoja na ticket ya atakaye kwenda pamoja na mwili ni dola elfu ishirini[$.20,000].Ni mzigo mkubwa sana ambao kila mmoja wetu anombwa kusadia ili kukamilisha shughuli hii hasa ukizingatia ya kuwa kwa kadri mwili unavyokaa funeral-home ndio gharama zinavyozidi kuongezeka.Mwili utasafirishwa punde zitakapopatikana fedha za kulipia gharama.Unaweza kutuma mchango wako kwenye Account ya wafiwa kama ifuatavyo:NAOMI  MEREREBANK OF AMERICA,ROUTE NUMBER :011000138ACCOUNT NUMBER:009441233628Au kwa adress hii:Jacob Anna Merere510 Skylinedrive suite # 11Dracut,MA 01826.Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na wafuatao:Jacob Anna Merere [JJ]-978-726-2227 au 978-957-2153.Naomi Merere-978-413-3722 au 978-632-9823.Juma Malika-781-244-7353Saimon Twalipo-978-423-1192Pastor Abisalom Nasua-214-554-7381Email-Adress:- RambiRambi@Yahoo.comTafadhali chukua muda kuwafariji wafiwa na kuwaombea Tunatanguliza shukrani kwa misaada yote iliyotolewa kuwasaidia familia Merere !Mbarikiwe,Mch.Abisalum Nasua,Jackson MollelMichango-Kwa Niaba ya Marafiki wa Familia ya Merere.Comments (7)Miongoni mwa habari za watu maarufu ambazo bila shaka zimegubika vichwa vya wengi wiki hii ni ile ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP,Reginald Mengi kukanusha taarifa za gazeti moja kwamba amefunga ndoa mpya na mwanamke mmoja wa jijini Dar-es-salaam(Lilian Kimaro) na kulaumu uandishi wa habari unaokwenda kinyume na misingi ya taaluma hiyo.Kwa habari zaidi unaweza kubonyeza hapa. Pia unaweza kubonyeza hapa ili kuona baadhi ya maswali ambayo waandishi wa habari walimbana nayo Mengi lakini akakwepa kwa kigezo kwamba wakatafute wenyewe ukweli!Photo/Venance NestoryComments (49)Anaitwa Maunda Zorro.Anatokea kwenye ile ile familia ya kina Zorro ambayo tunaweza kabisa kuiita Music Family .Tangu alipoingia rasmi kwenye fani ameshaachia nyimbo kadhaa ambazo sio tu zimeshika chati bali zimethibitisha kipaji alichonacho.Pamoja na uthibitisho wa kipaji,lipo swali ambalo bado sijalipatia majibu pamoja na kujaribu kulifanyia utafiti mara kadhaa;Hivi uimbaji(naongelea uimbaji mahiri ambao wengi tunaweza kukubaliana kwamba hapo sawa) ni kipaji mtu anazaliwa nacho au ni kitu ambacho yeyote anaweza kujifunza?Na mazingira anayokulia mtu yana mchango wa kiasi gani katika kipaji?Miongoni mwa nyimbo hizo ni huu hapa unaokwenda kwa jina Nataka Niwe WakoPhoto/A.Mrisho.Comments (17) Privacy Cookies: This site uses cookies. By continuing to use this website, you agree to their use. To find out more, including how to control cookies, see here: Cookie Policy

TAGS:You Wanted To 

<<< Thank you for your visit >>>

All You Wanted To Know But Didn't Know How and Where

Websites to related :
Fort Willow Archaeology St. Jos

  Fort Willow Archaeology St. Joseph s High School Archaeology Field School at Fort Willow, a War of 1812 site near Barrie, Ontario Welcome to Fort Will

日本建設機械工業会

  建設機械の成長アルバム数字で見る建設機械産業国際社会との共存共栄暮らしをささえる建設機械 災害からあなたを守る建設機械 終わりのない挑戦-安全なマシンの追

Family Recipes and Traditions |

  Easy recipes for dips, spreads, finger foods, and boards that are perfect for the start of any meal or party!Here are holiday and seasonal recipes to

Max Walker, Tangles, Public, Spe

  Max's kitbag of tools include his skill in being a... Certified Speaking Professional, Master Communicator, Corporate Connecter, Storyteller, Writer/A

Opportunity Desk Blog

  Everyone feels as though they just can t squeeze enough out of the day. You hit 10pm and wonder, Where has the time gone? If you feel like you don t g

Lal Baba- The Spiritual Guide |

  Aadhyatam Mahimahttp://www.aadhyatammahima.comThis gives me pleasure to inform peoples/my freinds/my associates from different fieldes that I Ashok Ku

Custom Gun Vaults | Fort Knox Va

  Let's find the right vault for you You have the advantage when you select a USA manufactured handcrafted vault. Select the home safe, gun safe, or sec

Modern Man | Mens Style, Gadgets

  Physical characteristics like long legs, medium-large breasts, and narrow waist play a vital...

iamabeautyjunkee | Product Revie

  Take took a look at the future of beauty: These are the most exciting anti-aging miracles and new skin-care gizmos that are in the pipeline. Coming so

Restoran Jerry Restoran Jerry N

  Na najekskluzivnoj lokaciji na Novom Beogradu nalazi se moderno koncipirani i luksuzno opremljen elitni restoran Jerry.Uvođenjem novih svetskih trend

ads

Hot Websites